##plugins.themes.academic_pro.article.main##

Abstract

Utafiti huu ulishughulikia uchunguzi wa matumizi ya vifaa vya ufundishaji wa msamiati wa kiswahili katika
shule za msingi za umma, Kaunti Ndogo ya Kisumu Mashariki, Kenya. Malengo aliyozingatia mtafiti katika
utafiti huu yalikuwa pamoja na kutambua changamoto zilizopo wakati wa kutumia vinyago, video na chati
katika somo la msamiati, kudadisi sera zilizopo za ukaguzi ili kudhibiti utumizi wa video, chati na vinyago ili
kusaidia uelewekaji wa msamiati na kuchunguza udhaifu na ufaafu uliopo katika ufundishaji msamiati kwa
kutumia video, chati na vinyago katika somo la Kiswahili. Utafiti ulilenga idadi ya walimu kumi wa
Kiswahili katika Shule za msingi katika Kaunti Ndogo ya Kisumu Mashariki. Baadhi ya hizi mtafiti aliteuwa
kwa bahati nasibu walengwa walioteuliwa kama hivi walimu wakuu kumi, walimu wa Kiswahili kumi na
wanafunzi kumi. Walengwa wote walikuwa mia nane ishirini ambao waliimbua asilimia kumi, basi idadi ilio
hojiwa ikawa themanini na wawili. Hojaji zilikuwa tatu za walimu wakuu, walimu wa Kiswahili. Utafiti
ulichanganuliwa kwa kutumia SPSS kuonyesha idadi katika alama za asilimia na uradidi. Baada ya kutafiti
na kuchanganua data, mtafiti alipendekeza haja ya walimu wa Kiswahili kuwa na vikao katika majopo.
Mtafiti pia aona kuwa kuna haja washika dau wote wa elimu kufufua taasisi za Kaunti ili kukuza hitaji la
uundaji visaidizi ili walimu wapate kuendeleze ueledi wao wa kuunda visaidizi ili kuboresha uelewekaji wa
dhana za Kiswahili. Kadhalika,washika dau wana changamoto kubwa ya kuleta mashuleni rasilimali ya
kutosha kutengeneza visaidizi vinavyohitajika. Jambo lingine ni kuwa shule zingetenga sehemu mahususi ya
kuhifadhi visaidizi ili vitumike bila uwoga wa kuharibika ama kupotea. Mwisho, walimu watie misingi thabiti
ya ufunzaji msamiati kuanzia madarasa ya chini ili wanafunzi wasielewe dhana hizi kimakosa kisha
wahitajike kurekebishwa baadaye. Jambo hili ndilo lililokita mizizi sehemu nyingi za Kaunti ya Kisumu
Mashariki, Kenya

##plugins.themes.academic_pro.article.details##

How to Cite
Kamau Hellen Wambui1 , Pro. Samson Odingi2 , Dr Hamisi Babusa3. (2016). Matumizi Ya Visaiddizi Vya Ufundishaji Msamiati Wa Kiswahili Katika Shule Za Msingi Za Umma, Kaunti Ya Kisumu Mashariki, Kenya. International Journal of Emerging Trends in Science and Technology, 3(10), 4671-4679. Retrieved from https://igmpublication.org/ijetst.in/index.php/ijetst/article/view/1227