##plugins.themes.academic_pro.article.main##

Abstract

Utafiti huu ulishughulikia uchunguzi wa matumizi ya vifaa vya ufundishaji wa msamiati wa kiswahili katika
shule za msingi za umma, Kaunti Ndogo ya Kisumu Mashariki, Kenya. Malengo aliyozingatia mtafiti katika
utafiti huu yalikuwa pamoja na kutambua changamoto zilizopo wakati wa kutumia vinyago, video na chati
katika somo la msamiati katika somo la Kiswahili. Utafiti ulilenga idadi ya walimu kumi wa Kiswahili katika
Shule za msingi katika Kaunti Ndogo ya Kisumu Mashariki. Baadhi ya hizi mtafiti aliteuwa kwa bahati nasibu
walengwa walioteuliwa kama hivi walimu wakuu kumi, walimu wa Kiswahili kumi na wanafunzi kumi.
Walengwa wote walikuwa mia nane ishirini ambao waliimbua asilimia kumi, basi idadi ilio hojiwa ikawa
themanini na wawili. Hojaji zilikuwa tatu za walimu wakuu, walimu wa Kiswahili. Utafiti ulichanganuliwa kwa
kutumia SPSS kuonyesha idadi katika alama za asilimia na uradidi. Baada ya kutafiti na kuchanganua data,
mtafiti alipendekeza haja ya walimu wa Kiswahili kuwa na vikao katika majopo. Vivyo, wataweza kujadili na
kutayarisha visaidizi wanavyohitajika kuboresha uelewekaji wa msamiati. Pamoja na hayo pia watauunda sera
za kutengeneza visaidizi vya somo la Kiswahili zitakazowawezesha kupanga mikakati ya kukaguana wao kwa
wao. Jambo hili litakuza umoja wa kufaana. Mtafiti pia aona kuwa kuna haja washika dau wote wa elimu
kufufua taasisi za Kaunti ili kukuza hitaji la uundaji visaidizi ili walimu wapate kuendeleze ueledi wao wa
kuunda visaidizi ili kuboresha uelewekaji wa dhana za Kiswahili. Kadhalika,washika dau wana changamoto
kubwa ya kuleta mashuleni rasilimali ya kutosha kutengeneza visaidizi vinavyohitajika. Jambo lingine ni kuwa
shule zingetenga sehemu mahususi ya kuhifadhi visaidizi ili vitumike bila uwoga wa kuharibika ama kupotea.
Mwisho, walimu watie misingi thabiti ya ufunzaji msamiati kuanzia madarasa ya chini ili wanafunzi wasielewe
dhana hizi kimakosa kisha wahitajike kurekebishwa baadaye. Jambo hili ndilo lililokita mizizi sehemu nyingi za
Kaunti ya Kisumu Mashariki, Kenya.

##plugins.themes.academic_pro.article.details##

How to Cite
mau Hellen Wambui1 , Pro. Samson Odingi2 , Dr Hamisi Babusa3. (2016). Matumizi Ya Visaiddizi Vya Ufundishaji Msamiati Wa Kiswahili Katika Shule Za Msingi Za Umma, Kaunti Ya Kisumu Mashariki, Kenya. International Journal of Emerging Trends in Science and Technology, 3(07), 4375-4385. Retrieved from http://igmpublication.org/ijetst.in/index.php/ijetst/article/view/1156